NI SIMBA SC NA AZAM FC TENA FAINALI MAPINDUZI KWA MARA YA TATU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NI SIMBA SC NA AZAM FC TENA FAINALI MAPINDUZI KWA MARA YA TATU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa penalti 3-1 dhidi ya Malindi SC usiku wa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Simba SC iliyotumia wachezaji wengi wa timu ya vijana leo, sasa itakutana na Azam FC katika Fainali ambayo mapema jioni ya leo iliichapa mabao 3-0 KMKM Uwanja wa Amaan, Zanzibar pia.
Baada ya dakika 90 ngumu, mabeki Yussuf Mlipili, Mghana Asante Kwasi na kiungo Mohammed ‘Mo’ ibrahim wakaifungia SImba SC penalti zao huku beki mpya, Zana Coulibaly kutoka Burkina Faso akikosa kwa kupiga juu.
Kwa upande wa Malindi, Abdulswamad Kassim pekee alifunga penalti yake, huku Ali Kani, Muharami Issa na Cholo Ali wakikosa wote.

Tukio la kusisimua katika mchezo huo ni pale beki wa kati wa Simba, Paul Bukaba alipovunja kioo cha chumba cha waandishi wa habari baada ya shuti lake akiokoa hatari langoni mwake kwenda moja kwa moja katika dirisha la chumba hicho dakika ya 76.
Katika mchezo uliotangulia jioni mabao y... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More