Ni vita ya Wababe wikendi hii kwenye Bundesliga - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ni vita ya Wababe wikendi hii kwenye Bundesliga

Kwa wapenzi wa soka kote duniani hakuna raha kama kuona timu mbili kubwa zikivaana Uso kwa Uso tena zikiwa na mashabiki lukuki. Miongoni mwa mechi za kusisimua sana katika Ulimwengu wa soka ni ile ya watani wa jadi wawili nchini Ujerumani, ni miamba wa jiji la Dortmund na wababe wa jiji la Munich. Borussia Dortmund vs Bayern Munich na Der Klassiker ndio jina halali la mchezo huo.Dortmund ambao wanaongoza ligi watakuwa nyumbani katika dimba la Signal Iduna Park Jumamosi hii tar 10, majira ya 2:30 saa za Afrika Mashariki, kuwakabili mabingwa wa ligi hiyo  msimu uliopita Bayern Munich.Mpaka sasa Dortmund hawajapoteza mchezo wowote katika Bundesliga msimu huu huku Bayern wao wakiwa wameshapoteza michezo miwili hadi sasa. Pia Dortmund waliambulia vipigo katika mechi tatu zilizopita za Der Klassiker, lakini wikendi hii wanayo nafasi ya kubadilisha  bahati yao kwani wanacheza kandanda safi msimu huu huku wapinzani wakionesha kutowepo katika kiwango kilichozoeleka kwa miaka kadhaa sasa.
Kwa w... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More