NI YANGA NA AZAM FC NA SIMBA SC NA MTIBWA SUGAR NUSU FAINALI LIGI KUU YA VIJANA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NI YANGA NA AZAM FC NA SIMBA SC NA MTIBWA SUGAR NUSU FAINALI LIGI KUU YA VIJANA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
YANGA SC itakutana na Azam FC katika Nusu Fainali ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, wakati mahasimu wao jadi, Simba SC watakutana na Mtibwa Sugar.
Hiyo ni baada ya mechi za mwisho za Kundi B leo,  Mtibwa Sugar na Azam FC zikigawana pointi kwa sare ya 1-1 na Tanzania Prisons ikiichapa 2-1 Biashara United.
Kwa matoko hayo, Mtibwa Sugar wanamaliaza kileleni mwa kundi hilo ikiwa na pointi saba sawa na Azam FC , lakini timu ya Manungu inakuwa juu kwa wastani wake mzuri wa mabao.

Tanzania Prisons wamemaliza nafasi ya tatu kwa pointi zao tatu na Biashara United wameburuza mkia wakiwa hawajaambulia pointi yoyote.... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More