NIDA YAANZA KUTOA VITAMBULISHO VYA UTAIFA KWA WALEMAVU KINONDONI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NIDA YAANZA KUTOA VITAMBULISHO VYA UTAIFA KWA WALEMAVU KINONDONI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo amezindua rasmi zoezi la utambuzi na usajili kwa watu wenye ulemavu ili waweze kupata vitambulisho vya utaifa na hii ni kwa kushirikiana na mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) na ofisi ya ustawi wa jamii Wilayani humo.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ameipongeza mamlaka hiyo na ofisi ustawi wa jamii Kinondoni kwa kuwajali watu wenye mahitaji maalumu na kuandaa jukwaa maalumu la kuwatambua na kuwasajili na kutoa vitambulisho vya utaifa.

Amesema kuwa vitambulisho hivyo vitawasaidia katika kupata huduma mbalimbali ya kijamii na amewataka wanajamii kuwahimiza na kuhakikisha kila mtu mwenye ulemavu wa aina yoyote anapata huduma hiyo ya utambuzi na usajili na kupatiwa kitambulisho chake cha utaifa.

Aidha Chongolo amewahaidi walemavu hao kuwapatia fungu la fedha lililopo katika bajeti ya serikali ili waweze kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.

Kwa upande wake Afisa msajili (NIDA) Wilaya ya Kinondoni ... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More