NIDA YAENDELEA KUWAHIMIZA WANANCHI KUJISAJILI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NIDA YAENDELEA KUWAHIMIZA WANANCHI KUJISAJILI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MAMLAKA ya vitambulisho vya taifa (NIDA) imeendelea kuwahimiza wananchi kujiandikisha ili waweze kupata vitambulisho vya utaifa ambavyo umuhimu na matumizi yake kwa sasa yamekuwa makubwa zaidi.
Akizungumza na blogu ya jamii Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya mamlaka hiyo Rose Mndeme amesema kuwa wanataraji  kufikia malengo ya wananchi wanaosajiliwa kukidhi vigezo vya uraia (Watanzania) na wanakidhi vigezo vingine  hasa sehemu zao za makazi.
Amesema kuwa umuhimu za zoezi la mapingamizi na uhakiki wao kama mamlaka hawawezi kuwajua Watanzania wote hivyo Watanzania lazima wawe wazalendo kwa taifa letu kwani wakiruhusu wageni kujiandikisha watawapa fursa ya kumiliki ardhi na kuleta athari nyingine kama hizo.
Aidha amesema kuwa mamlaka hiyo kwa mkoa wa Dar es salaam bado wanaendelea kutoa vitambulisho kwa wananchi waliojisajili muda mrefu hivyo wananchi wafuate vitambulisho vyao katika ofisi za kata walizojiandikisha  na kuvihifadhi vizuri.
Akieleza umuhimu w... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More