Nikki wa Pili Aunga Mkono Makatazo ya Kucha na Kope Bandia. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Nikki wa Pili Aunga Mkono Makatazo ya Kucha na Kope Bandia.

Mwanamuziki wa hip -hp nchini Niki wa Pili ameunga mkono maagizo ya spika wa bunge ya kuwakataza wabunge kuingia bungeni wakiwa na kucha bandia na kope bandia ilhali wanakwenda kwa ajili ya kuwakilisha wananchi waliowaamini.


Niki anasema kuwa amefurahishwa na uamuzi huo kwasababu hata yeye ni moja kati ya wale wanaopenda sana urembo ailia kuliko ule urembo wa bidhaa hivyo anaona ni uamuzi sahihi kwa sababu wanawake wanatumia bila kujua madhara yake ya baadae.


mimi napenda sana urembo asilia na ndiomaana ninamuunga mkono sana spika wa bunge,lakini pia nafikiria kwa hadhi ya bunge spika ametumia uamuzi mzuri sana kwa sababu naona kama walikuwa wanavuka mipaka.Watu wanatakiwa kujua madhara ya vitu bandia  maana mwili wa binadamu umegeuka kuwa bidhaa kwa sasa.


Niki anasema kuwa kwa sasa mwili wa binadamu umekuwa bidhaa kiasi kwamba ukienda madukani unakutana na nywele bandia, kucha bandia, na hata vifaa vya kubadilisha ngozi rangi.


 


The post Nikki wa Pili Aunga Mkono Makatazo ya Kucha n... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More