NIMR yatakiwa kuongeza ufanisi - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NIMR yatakiwa kuongeza ufanisi

Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), imetakiwa kuboresha ukusanyaji wa takwimu katika magonjwa ya mlipuko ikiwemo dengue na kipindupindu, ili kusaidia kutambua idadi halisi ya wagonjwa pamoja na vifo vinavyotokea katika jamii hali itayosaidia kuboresha utoaji huduma nchini.


Akiwa katika ziara ya kuitembelea taasisi hiyo, Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile, amesema kwa sasa taasisi hiyo inapaswa kuongeza nguvu ya utendaji kazi, hususani katika tafiti za magonjwa yasiyoambukizwa na yanayoambukiza, kwani kufanya hivyo itasaidia kupata njia ya kukabiliana na magonjwa hayo.


Aidha, amesema ni muhimu kwa taasisi hiyo kushirikisha viongozi wa kisera katika shughuli zao ili kutambua mafanikio na changamoto za taasisi hiyo, jambo litakalorahisisha kutatua changamoto zinazoikumba taasisi hiyo.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa NIMR, Profesa Yunus Mgaya, amemshukuru Dk Ndugulile kwa kufanya ziara katika Taasisi hiyo na ameahidi kutekeleza maagizo yote ndani ya muda mfupi.Tweet... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More