Nipo Tayari Kuzaa Wakati Wowote Sasa- Sanchi - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Nipo Tayari Kuzaa Wakati Wowote Sasa- Sanchi

Socialite na mwanamitindo maarufu nchini mwenye umbo la aina yake Jane Rimoy maarufu kama Sanchi amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya kuzaa hivi karibuni.


Sanchi ameweka wazi nia yake ya kumpa mjukuu mama yake mzazi kwani anaamini kumpa mjukuu ndio zawadi pekeee ambayo inaweza kumfurahisha mama yake.


Kwenye mahojiano  na gazeti la Ijumaa Wikienda, Sanchi alisema kuwa mama yake amekuwa na hofu kutokana na kazi yake ya uanamitindo na kuzunguka nchi mbalimbali kwamba itakuwa ngumu kwake kuweza kutulia na kubeba ujauzito mpaka kujifungua.“Kwa kweli niko mbioni kumpa mama yangu zawadi ya mjukuu maana amekuwa na wasiwasi sana kutokana na kazi yangu ninayofanya anaona labda nitachelewa sana kumpatia mjukuu hivyo nataka kwenye hilo nisimuangushe nalifanyia kazi”. 


The post Nipo Tayari Kuzaa Wakati Wowote Sasa- Sanchi appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More