Nisha- Biashara Zimenipa Mafanikio Kuliko Filamu - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Nisha- Biashara Zimenipa Mafanikio Kuliko Filamu

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Salma Jabu maarufu kama Nisha amedai biashara zake za nguo zimeweza kumpatia mafanikio ya haraka ambapo mpaka sasa tayari ameshanunua nyumba na magari ya kutembelea.


Nisha amefunguka Kwenye mahojiano na Bongo 5 na kuweka wazi kuwa alipokuwa anafanya Bongo Movie alikuwa anapata pesa ndogo ndogo sana ambazo aliziweka na kuanzisha biashara yake kuuza nguo ambayo amekiri kuwa imempa mafanikio mengi sana.Mimi filamu nimeanza kucheza kama hausegirl nikilipwa sana labda elfu ishirini lakini pesa hiyo hiyo ndio imenipa leo hii biashara yangu ya nguo ambayo inanifanya mimi kila siku niende benki kwenda kuweka pesa”.Lakini pia Nisha ameanika mali zake alizozipata Kupitia biashara zake.:Kwa kweli mimi nina nyumba nina magari kama unavyoona nimepaki jingine pale nje kwaiyo namshukuru Mungu biashara zangu ndio zimenipa mafanikio sana”. 


 


The post Nisha- Biashara Zimenipa Mafanikio Kuliko Filamu appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More