Nisha: Sitoweza Msahau Mzee Majuto Maishani - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Nisha: Sitoweza Msahau Mzee Majuto Maishani

Msanio wa filamu za kibongo na msanii wa Bongo fleva Salma Jabu maarufu kama Nisha amefungukia Kifo Cha Msanii mwenzake mkongwe wa Bongo movie na comedy Mzee Majuto aliyeaga dunia wiki iliyopita.


Nisha amefunguka na kudai yupo katika majonzi mazito katika kipindi hiki ambacho Msanii huyo Nzee Majuto amefariki dunia kwani pengo alilomuachia haliwezi kuzibika katu.


Kwenye mahojiano na Global Publishers, Nisha alieleza kuwa, kifo cha Mzee Majuto kimemuumiza kupitia kiasi na pengo alilomwachia moyoni mwake ni kubwa kwani mashabiki wa filamu hasa za vichekesho wasingemjua.Mzee Majuto nilikuwa namwita baba kwa sababu amenitoa kisanaa, yaani alikuwa ni kiungo muhimu sana maishani mwangu, machozi na maumivu yangu havitafutika, nashindwa kuamini na pengo lake halifutiki maishani mwangu”.Mzee Majuto alifariki dunia siku chache zilizopita katika hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mrefu.


The post Nisha: Sitoweza Msahau Mzee Majuto Maishani appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More