njia pekee ya kulipa wema kwa wananchi ni viongozi wake kufanya kazi kwa bidii na ubunifu-ccm - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

njia pekee ya kulipa wema kwa wananchi ni viongozi wake kufanya kazi kwa bidii na ubunifu-ccm

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) ndugu Humphrey Polepole amesema njia pekee ya CCM kulipa wema kwa wananchi ni viongozi wake kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ili kuleta maendeleo endelevu nchini. 
Amesema wananchi wamekiamini Chama na kukipa ridhaa ya kuongoza Serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutokana na usimamizi na utekelezaji mzuri wa Sera zake kwa jamii. Rai hiyo aliitoa leo (jana) katika hafla ya kukabidhi mipira ya kusambazia maji safi na salama kwa wananchi wa Jimbo la Tunguu huko katika ukumbi wa T.C uliopo Dunga Wilaya ya Kati Unguja. 
Akizungumza mara baada ya kukabidhi mipira hiyo kwa uongozi wa Jimbo la Tunguu kwa niaba ya wananchi, Ndugu Polepole amesifu juhudi za kuwatumikia wananchi zinazofanywa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo.Polepole aliwataja viongozi hao ambao ni Mbunge wa Jimbo hilo Khalifa Salum Said na Mwakilishi wa Jimbo hilo Simai Mohamed Said kuwa wam... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More