NMB WADHAMINI MASHINDANO YA GOLF YA MKUU WA MAJESHI, JWTZ - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NMB WADHAMINI MASHINDANO YA GOLF YA MKUU WA MAJESHI, JWTZMkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akimkabidhi moja ya jezi Mwenyekiti wa klabu ya gofu Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo zilizotolewa na NMB ikiwa ni sehemu ya udhamini wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi nchini yanayotarajia kufanyika Oktoba 13 katika viwanja vya Lugalo Dar es Saalam.

BENKI ya NMB imedhamini Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi nchini yanayotarajia kufanyika Oktoba 13 na kushirikisha wachezaji wa gofu kutoka klabu mbalimbali nchini.

Udhamini uliotolewa ni wa shilingi milioni 26 pamoja na vifaa mbalimbali zikiwemo jezi zitakazo tumika katika mashindano hayo vimekabidhiwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Omari Mtiga katika viwanja vya Lugalo.Kukabidhiwa kwa udhamini huo ni mwendelezo wa Benki ya NMB kudhamini na kusaidia shughuli anuai za michezo hususani ya Jeshi la wananchi.

Akizungumza na mwandishi wa... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More