NMB YASAIDIA VITANDA 9 KITUO CHA AFYA KIGAMBONI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NMB YASAIDIA VITANDA 9 KITUO CHA AFYA KIGAMBONI


BENKI ya NMB imetoa msaada wa vitanda tisa vya wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Kigamboni vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni tano. Vitanda hivyo sita (6) vikiwa vya wagonjwa wa kawaida na vitatu (3) vikiwa maalum kwa ajili ya kujifungulia kwa wajawazito, vimekabidhiwa leo kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija.

Akikabidhi vitanda hivyo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd alisema msaada huo ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa NMB kurejesha faida kidogo kwa jamii. Alisema Benki hiyo, hutenga takribani bilioni moja fedha ambayo hurejesha kwa jamii kwa kusaidia sekta za afya, elimu na masuala mengine yanayoikumba jamii kama maafa na majanga.

Alisema Benki ya NMB inaunga mkono juhudia za Serikali za kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo afya kwa wananchi, ili jamii ambao ni sehemu ya wateja wa benki hiyo wawe na afya njema."..Kama tunavyojua afya ni huduma ya msingi kwa jamii wakiwemo wate... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More