NSSF YAJIPANGA KUPELEKA TAIFA KWENYE UCHUMI WA VIWANDA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NSSF YAJIPANGA KUPELEKA TAIFA KWENYE UCHUMI WA VIWANDA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
SHIRIKA la taifa la hifadhi ya jamii (NSSF) limeshiriki katika maonesho ya tatu ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yaliyozinduliwa rasmi leo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam kwa kutoa huduma kwa wajasiriamali ikiwa ni mchakato kwa kukamilisha azma ya ujenzi wa Tanzania ya viwanda.
Akizungumza na blogu ya jamii Afisa mwandamizi kitengo cha sekta isiyo rasmi  (NSSF) Abas Cothema amesema kuwa, wameungana na shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO)  katika maonesho hayo ya bidhaa za viwanda zinazozalishwa nchini ikiwa ni  kuunga mkono  jitihada za Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli iliyodhamiria kujenga Tanzania ya viwanda.
Amesema kuwa NSSF imeshiriki maonesho hayo ili kuhakikisha wanawapatia hifadhi ya jamii wajasiriamali ili waweze kukingwa dhidi ya majanga yanayosababisha  upotevu wa kipato na kuwapa pensheni ya uzeeni, pensheni ya ulemavu, pensheni ya  urithi na bima ya afya ambazo ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More