Nuh Mziwanda Alivunja Mahusiano Yangu na Prezzo- Amber Lulu - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Nuh Mziwanda Alivunja Mahusiano Yangu na Prezzo- Amber Lulu

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na video vixen maarufu Lulu Eugene ‘Amber Lulu’ amefunguka na kudai kuwa Msanii wenzake Nuh Mziwanda ndiye sababu kubwa ya Penzi lake na Prezzo kufa.


Amber Lulu na Prezzo walikuwa Kwenye Mahusiano ya muda mrefu lakini mapenzi yao yaliingia doa mara baada ya video iliyomuonyesha Nuh Mziwanda na Amber Lulu wakifanya yao kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.


Kwenye mahojiano aliyofanya  katika kipindi cha The Playlist cha Times FM, Amber amekiri kuwa kuna kipindi alikuwa karibu na Nuh Mziwanda na baadaye picha zake zilisambaa mitandaoni  wakiwa karibu wakijiachia kimahaba.NUH NI MSHIKAJI TU ILA NDOA YANGU NA PREZZO ALIMAIND ILE KUKISIANA KISIANA NA NUH MZIWANDA JAPO NI MAKOSA TU KWAKUWA MIMI NI KIJANA NA YEYE YUPO MBALI MI NIPO HUKU MUDA MWINGINE NAHITAJI VITU VINGI LAKINI KUTELEZA KUPO  ILA NILIJITAHIDI SANA KUOMBA MSAMAHA SANA NIKAONA KAMA KANIKAZIA HIVI MWISHO WA SIKU NIKAONA NAOMBA MSAMAHA SANA KWAAJILI YA NINI NIKAONA FRESH TU KAMA UMEAMUA POA ... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More