NYOTA WA AZAM FC, FRANK DOMAYO NA PAUL PETER WAPELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

NYOTA WA AZAM FC, FRANK DOMAYO NA PAUL PETER WAPELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
NYOTA wawili wa Azam FC, kiungo Frank Domayo na mshambuliaji Paul Peter wameondoka jioni ya leo kwenda mjini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.
Majeruhi hao wawili wameondoka wakiongozan na Mtendaji Mkuu wa klabu, Abdulkarim Amin ‘Popat’  kwa ajili ya kwanza kwenda kufanyiwa uchunguzi na baadaye matibabu.
Wakati Paul Peter aliumia akiicheza timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes Aprili mwaka huu, Domayo anayejulikana kwa jina la utani ‘Chumvi’ aliumia jana kwenye mazoezi ya timu ya taifa, Taifa Stars iliyokuwa ikijiandaa kwa mechi na Cape Verde.

Frank Domayo (kulia) akiwa na Paul Peter leo wakati wa safari yao kwenda Cape Town 

“Wote wawili wameumia magoti wakitetea Taifa, Uongozi wa Azam umeamua wakafanyiwe matibabu Afrika Kusini, hivyo basi wanaondoka leo alasiri na ndege ya shirika la Afrika Kusini kwenda katika hospitali ya Mtakatifu Vincent Palloti,”amesema, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim A... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More