OBREY CHIRWA AANZA KAZI KWA KISHINDO AZAM FC, AKUTANA TENA NA PACHA WAKE WA TANGU PLATINUMS, DONALD NGOMA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

OBREY CHIRWA AANZA KAZI KWA KISHINDO AZAM FC, AKUTANA TENA NA PACHA WAKE WA TANGU PLATINUMS, DONALD NGOMA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI mpya wa Azam FC, Obrey Chirwa, leo asubuhi ameanza kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza kwenye timu yake hiyo mpya.
Staa huyo wa zamani wa Yanga SC ya Dar es Salaam na FC Platinum ya Zimbabwe, amejiunga na Azam FC akitokea Nogoom ya Misri kwa usajili huru baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na timu hiyo.
Chirwa amejumuika mazoezini kwa mara ya kwanza na wenzake, wakati timu hiyo ikianza rasmi kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) dhidi ya Ruvu Shooting utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Novemba 22 mwaka huu.
Obrey Chirwa akiwa mazoezini na timu yake mpya, Azam FC leo asubuhi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam 
Obrey Chirwa akifanya mazoezi kwa bidii leo asubuhi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam 
Obrey Chirwa amekutana tena na mchezaji mwenzake wa zamani wa FC Platinums ya Zimbabwe na Yanga SC, Donald Ngoma
Obrey Chirwa atafanya kazi tena na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm wali... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More