OBREY CHIRWA AANZA KUJIFUA AZAM FC - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

OBREY CHIRWA AANZA KUJIFUA AZAM FC

Na Zainab Nyamka, Globu ya JamiiMSHAMBULIAJI mpya wa Klabu ya Azam FC, Obrey Chirwa, leo asubuhi ameanza kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza kwenye timu yake hiyo mpya.
Staa huyo wa zamani wa Yanga na FC Platinum, amejiunga na Azam FC akitokea Nagoon ya Misri kwa usajili huru baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na timu hiyo.
Chirwa amejumuika mazoezini kwa mara ya kwanza na wenzake, wakati timu hiyo ikianza rasmi kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) dhidi ya Ruvu Shooting utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Novemba 22 mwaka huu.
Kwa mara nyingine tena Cirwa anaungana na rafiki yake wa siku nyingi, Donald Ngoma, ambaye walicheza naye Platinum ya Zimbabwe kwa takribani miaka sita kabla ya kufanya tena kazi pamoja wakiwa Yanga na sasa Azam FC, mara zote mbili hapa Tanzania wakiunganishwa na Kocha Mkuu, Hans Van Der Pluijm, ambaye kwa sasa anaifundisha Azam FC.
Mazoezi hayo yaliyosimamiwa na Kocha Pluijm, yalikuwa ni makali lengo kuu ni kurudisha ufiti kwa wache... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More