OFISA WA KODI TRA , POLISI WAWILI KORTINI KWA TUHUMA ZA KUOMBA RUSHWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

OFISA WA KODI TRA , POLISI WAWILI KORTINI KWA TUHUMA ZA KUOMBA RUSHWA

*Ni wale waliotajwa wakati wa kikao cha Rais Magufuli na wafanyabiashara
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
OFISA Msaidizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato nchini(TRA) Charity Ngalaw(28) na askari Polisi wawili wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na shtaka la kuomba rushwa ya Sh. Milioni mbili.
Mbali Ngalawa, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Askari Polisi wa kituo cha Polisi Osterbay, H 4810 PC Ramadhani Uweza (28) na H 48 86 PC Simon Sugu (26).
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali kutoka Takukuru , Sofia Ngula amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa, Oktoba 29,mwaka 2016 huko Kimara Mwisho ndani ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam washtakiwa hao walishawishi rushwa ya Sh. Milioni mbili kutoka kwa mfanyabiashara wa Karikaoo jijini hapa, Ramadhani Ntunzwe , ili iwe kishawishi cha kuachia mizigo ya Mfanyabiashara huyo.
Kwa madai kuwa waliukamatwa kwa madai ya kufanya udanganyifu wa bidhaa al... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More