OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAWATAKA WAAJIRI NCHINI KUWAPATIA HUDUMA STAHIKI WATUMISHI WA UMMA WENYE ULEMAVU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAWATAKA WAAJIRI NCHINI KUWAPATIA HUDUMA STAHIKI WATUMISHI WA UMMA WENYE ULEMAVU

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetoa wito kwa waajiri nchini, kuwapatia huduma stahiki watumishi wa umma wenye ulemavu kwa mujibu wa Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma wenye Ulemavu wa mwaka 2008 kwa lengo la kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko wakati wa kikao kazi  cha Watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi cha kuadhimisha Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dodoma. Bi. Mwaluko amesema, walemavu kama walivyo binadamu wengine, wana wajibu wa kutoa mchango katika maendeleo ya taifa, hivyo ni wajibu wa waajiri wote nchini kuwapatia huduma zinazostahili ili waweze kutimiza wajibu wao.
Bi. Mwaluko amefafanua kuwa, watumishi wa umma wenye ulemavu hawana tofauti na watumishi wengine isipokuwa wana mahitaji yao ya msingi ambayo usipowapatia yanakwamisha utendaji kazi wao, hi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More