OKWI MCHEZAJI BORA LIGI KUU MWEZI OKTOBA NA PLUIJM AMBWAGA PATRICK J AUSSEMS WA SIMBA KUWA KOCHA BORA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

OKWI MCHEZAJI BORA LIGI KUU MWEZI OKTOBA NA PLUIJM AMBWAGA PATRICK J AUSSEMS WA SIMBA KUWA KOCHA BORA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi wa Simba SC ya Dar es Salaam ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo imesema kwamba, Okwi amekuwa Mchezaji Bora wa Oktoba baada ya kuwapiku Eliud Ambokile wa Mbeya City ya Mbeya na Yahya Zayed wa Azam FC ya Dar es Salaam pia. 
Okwi anakuwa mchezaji bora wa tatu wa msimu, baada ya mchezaji mwenzake wa Simba SC, Meddie Kagere kushinda tuzo ya Agosti na Ambokile kunyakua ya Septemba. 
Emmanuel Okwi wa Simba SC yameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi mwezi Oktoba
Mholanzi Hans van der Pluijm ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa mwezi Oktoba Ligi Kuu

Aidha, taarifa hiyo imesema kwamba Kocha wa Azam FC, Mholanzi Hans van der Pluijm ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa mwezi Oktoba baada ya kuiwezesha klabu yake kuongoza ligi hiyo.
Pluijm, kocha wa zamani wa Yanga ya Dar es Salaam pia na Singida United ya Singida, amewashinda Kocha Mkuu ... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More