OKWI, TSHISHIMBI, KUTINYU NA CHIRWA WABANANISHWA NA WAZAWA 11 TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MSIMU LIGI KUU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

OKWI, TSHISHIMBI, KUTINYU NA CHIRWA WABANANISHWA NA WAZAWA 11 TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MSIMU LIGI KUU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
WACHEZAJI wa kigeni, Mzimbabwe Tafadzwa Kutinyu, Mzambia Obrey Chirwa, Papy Kabamba Tshishimbi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Waganda Shafiq Batambuze na Emmanuel Okwi ni miongoni mwa wachezaji wachezaji 15 walioteuliwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika sherehe zitakazofanyika Juni 23 mwaka huu.
Kutinyu, Batambuze wa Singida United, Chirwa, Tshishimbi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Okwi wa Simba SC watachuana na wachezaji wengine 11 wazawa ambao ni Kelvin Yondani wa Yanga, Mudathir Yahya wa Singida United, Adam Salamba wa Lipuli, Habibu Kyombo wa Mbao FC, John Bocco, Shiza Kichuya na Erasto Nyoni wa Simba, Marcel Kaheza wa Maji Maji), Yahya Zaid wa Azam na Hassan Dilunga wa Mtibwa Sugar.

Licha ya Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL, pia siku hiyo katika sherehe zitakazofanyika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam kutatolewa tuzo mbalimbali ikiwemo ya Bingwa wa VPL, Mshindi wa Pili, Mshi... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More