OLE MILLYA AFAGILIA MIRADI YA KIMKAKATI YA MAGUFULI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

OLE MILLYA AFAGILIA MIRADI YA KIMKAKATI YA MAGUFULI


Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya amesema miradi mikubwa mitano ya kimkakati inayotekelezwa na iliyoahidiwa na Serikali ya Rais John Magufuli Wilayani Simanjiro ndiyo imesababisha yeye aondoke Chadema na kuhamia CCM.
Ole Millya akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Orkesumet alisema aliamua kuhama kama shukrani na kumuunga mkono Rais Magufuli kutokana na maendeleo hayo. 
Alitaja miradi hiyo ya maendeleo ni baada ya kusoma ilani ya CCM chini ya serikali ya Rais John Magufuli juu ya ujenzi wa barabara ya lami ya Arusha, Komolo, Terrat na Mirerani, Orkesumet, Kiteto hadi Kongwa mkoani Dodoma. 
Alisema mradi mkubwa wa maji wa mto Pangani (Ruvu) hadi Orkesumet wenye thamani ya sh41 bilioni unaoendelea, ukuta wa madini ya Tanzanite ambapo badala ya kukusanya sh70 milioni kwa mwaka sasa inakusanywa sh2.1 bilioni na wananchi wanafaidika nayo. 
"Mradi mwingine ni katika hospitali mpya 60 nchi nzima zinazojengwa na sisi Simanjiro tumepata hospitali ya wilaya tukitenge... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More