OLE NASHA ATOA AGIZO KALI KWA VIONGOZI NA WAZAZI MKOANI MANYARA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

OLE NASHA ATOA AGIZO KALI KWA VIONGOZI NA WAZAZI MKOANI MANYARA

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa William Ole Nasha amewataka viongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi vijiji nchini kote kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza darasa la saba hawaondoki katika maeneo yao kwenda kufanya kazi za ndani wakati wakisubiri matokeo ya kuhitimu darasa la saba, kwani kufanya hivyo kunawaondolea fursa ya kuendelea na masomo pindi wanapofaulu.
Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Manyara wakati akizungumza na viongozi hao kuhusu hali ya Elimu mkoani humo ambapo amewataka kusimamia kwa ukaribu suala hilo ili kutokatisha ndoto za watoto hao na kwamba wale wanaofanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

“Hakikisheni watoto wanaposubiri matokeo hawasafirishwi kwani wanapofika huko wanarubuniwa na waajiri hivyo hata matokeo yakitoka na kuonesha kuwa wamefaulu hawarejei kuendelea na masomo “alisisitiza Naibu waziri Ole Nasha.

Kiongozi huyo ameendelea kuwasisitiza wazazi kuwa fursa za Elimu katika nchi yetu ni kubwa, ikizingatiwa k... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More