Ommy Dimpoz atoa ujumbe mzito siku yake ya kuzaliwa ‘tusiishi kwa chuki na uadui’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ommy Dimpoz atoa ujumbe mzito siku yake ya kuzaliwa ‘tusiishi kwa chuki na uadui’

Alhamisi hii 13th September ni siku ya kuzaliwa ya mwanamuziki Ommy Dimpoz ambaye anafanya vizuri katika tasnia ya muziki nchini Tanzania.


Muimbaji huyo ambaye upo chini ya RockStar 40000, ameitumia siku yake hiyo kuandika ujumbe mzito kuhusu alichopitia kwenye maisha yake baada ya kupata matatizo katika mfuno wake wa kumeza chakula na kusababisha kufanyiwa upasuaji mkubwa nchini Afrika Kusini.


Ommy kupitia Instagram yake ameandika, “Leo 13th September ni kumbukumbu yangu ya siku ya kuzaliwa.Namshukuru sana Mwenyezi Mungu (ALHAMDULILAAH) kwa kunipa nafasi ya kuuona mwaka mwingine, kwani niliyoyapitia katika kipindi cha takribani miezi 5 kama ingekuwa sio mapenzi yake yeye (M/Mungu) basi ingekuwa imebaki history.

Nilichojifunza kipindi hichi chote ni kuwa kuumwa ni Ibada na sisi kama binadamu hatujakamilika leo unaweza kuwa mzima na kesho ukawa mahututi kitandani, ndio maana nimeamua kushare picha ambayo nilipigwa nikiwa ICU japo nafahamu sio kitu kizuri kupost picha kama hii kwenye mi... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More