Ommy Dimpoz atoka Afrika Kusini kwenye matibabu na kutua Kenya akiwa mwenye afya njema, abadilisha muonekano (+picha) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ommy Dimpoz atoka Afrika Kusini kwenye matibabu na kutua Kenya akiwa mwenye afya njema, abadilisha muonekano (+picha)

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz ambaye kwa miezi miwili amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya koromeo, hatimaye msanii huyo amepona kabisa kwa ushahidi wa picha alizopiga akiwa nchini Kenya.


Ommy Dimpoz

Kwa mujibu wa kinyozi maarufu nchini Kenya, George Dufanda ameposti picha za msanii huyo akiwa katika muonekano tofauti kabisa lakini mwenye uso wa tabasamu.


Maelezo kutoka kwa watu wanaofanya kazi karibu na Ommy Dimpoz wamesema msanii huyo amewasili nchini Kenya wiki moja iliyopita ma ameahidi kufanya Birthday Party yake nchini humo Septemba 17.


Bado haijajulikana kwa nini Ommy Dimpoz hajafikia Tanzania nyumbani kwake moja kwa moja. Tazama picha zake akiwa na kinyozi huyo maarufu nchini Kenya.Ommy Dimpoz akiwa na kinyozi aliyemnyoa

Ommy Dimpoz wiki mbili zilizopita alirudishwa tena nchini Afrika Kusini akitokea Tanzania kwa kutazamwa maendeleo ya afya yake baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa koromeo miezi miwili iliyopita.


The post Ommy Dimpoz atoka Afrika Kusini kwenye m... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More