ONGEZEKO WAHITIMU CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU DUCE NI MAFANIKIO- PROF KILLIAN - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ONGEZEKO WAHITIMU CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU DUCE NI MAFANIKIO- PROF KILLIAN

Na Zanab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mahafali ya kumi na moja (11) ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yamefanyika jana kwa jumla ya wahitimu 1769 wametunukiwa katika ngazi mbalimbali.
Kwenye mahafali hayo wahitimu 1736 wametunukiwa digrii za awali katkka fani mbalimbali, 26 wakitunukiwa stashada ya uzamili katika elimu na 7 wakitunukiwa shahada ya umahiri.
Akitoa hotuba kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es salaam Dkt Jakaya Mrisho Kikwete , Rasi wa Chuo Kikuu Kishirikishi Professa Bernadeta Killian amesema kuwa kati ya wahitimu wote wa mwaka huu wanaume ni 1255 na wanawake ni 514.
Amesema idadi ya wahitimu kwa upande wa digrii za awali ni kubwa ikilinganishwa na wahitimu wa miaka yote iliyopita, kwani wahitimu wa digrii za awali kwa mwaka 2017 ilikua ni 1443 ambalo ni ongezeko la wahitimu 239 na kufikia 1736 na wahitimu wa masomo ya sayansi kuongezeka mara mbili kutoka 231 kwa mwaka 2017 kufikia 472 kwa mwaka 2018.Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Dkt Jakaya Kikwete akitoa cheti k... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More