OSCAR MILAMBO NDIYE MKURUGENZI MPYA WA UFUNDI TFF, MADADI SASA MKURUGENZI WA MASHINDANO - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

OSCAR MILAMBO NDIYE MKURUGENZI MPYA WA UFUNDI TFF, MADADI SASA MKURUGENZI WA MASHINDANO

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ua umri wa miaka 17, Oscar Milambo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Uteuzi huo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya TFF, baada ya kumhamishia Salum Madadi aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi katika nafasi ya Mkurugenzi wa Mashindano.
Uamuzi huo umetolewa sambamba na maamuzi ya kumthibitisha Kidao Wilfred kuwa Katibu Mkuu wa TFF katika kikao kilichofanyika Julai 12, mwaka huu makao makuu ya TFF Karume, Ilala mjini Dar es Salaam.
Rais wa TFF Wallace Karia aliwasilisha suala la Kidao kwenye kikao hicho na Wajumbe kulipitisha na kuthibitisha rasmi Kidao katika nafasi hiyo.

Oscar MIlambo (katikati) ndiye Mkurugenzi mpya wa Ufundi wa TFF

“Kamati ya utendaji pia imemthibitisha Salum Madadi kuwa Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF.  Nafasi ya Madadi aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi iliyobaki wazi kamati ya utendaji imemthibitisha Kocha Oscar Mirambo kukaimu,”imesema taarifa ya TFF... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More