Pamba SC kuikabili Kagera Sugar CCM kirumba - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Pamba SC kuikabili Kagera Sugar CCM kirumba

Klabu ya Pamba Fc leo watashuka dimba la CCM Kirumba kupambana na Klabu inayoshiriki ligi kuu bara Kagera Sugar inayonolewa na Mecky Mexime.


Pamba Fc ambao ni Mabingwa mara moja ligi kuu Tanzania mwaka 1990 na mabingwa mara mbili wa Nyerere Cup ambapo kwa sasa linajulikana kama Azam Federetion Cup mwaka 1989 na 1992 watashuka dimba leo muda wa saa 10 katika dimba hilo kwa kiingilio cha 2000 tu.


Maendeleo ya soka kanda ya ziwa?


Msemaji wa chama cha Soka mkoa wa Mwanza amesema sasa hamasa ya soka kanda ya ziwa na Mwanza kwa ujumla imeongezeka kwa kiasi kikubwa baada ya mwenendo wake kudidimia. Kwa sasa ni vilabu viwili inayowakilisha jiji la Mwanza nayo ni Alliance Football Club na Mbao FC.Kwa mara ya kwanza kanda ya ziwa imetoa na vilabu takribani 6 kishiriki ligi kuu.


Biashara, Alliance, Mbao, Mwadui, Stand United na Kagera Sugar.


Klabu ya Mbao imefanikiwa kwa kiasi kupambana kubaki ligi kuu ili kulinda heshima ya jiji la Mwanza ambayo haoo awali iliwekwa na Pamba SC kwa kushiriki l... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More