PANAFRICAN ENERGY TANZANIA YASAINI MKATABA WA KUFADHILI UJENZI MIRADI YA AFYA WILAYA YA KILWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

PANAFRICAN ENERGY TANZANIA YASAINI MKATABA WA KUFADHILI UJENZI MIRADI YA AFYA WILAYA YA KILWA

Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imesaini mkataba wa ujenzi wa Kituo cha Afya Somanga na upanuzi wa hospitali ya Wilaya Kinyonga.

Mkataba huo wenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia mbili (1.2bilion) umesainiwa kati viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa na kampuni ya Pan African Energy ambao ni wadau wa maendeleo katika Wilaya ya Kilwa. Utiaji saini huo umeshuhudiwa na wawakilishi wa kampuni ya Pan African na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Ndg. Renatus Mchau ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo uliokuja kwa wakati na kueleza kuwa kwa muda mrefu Wilaya ya kilwa ilikuwa na changamoto katika sekta ya Afya lakini kwa sasa changamoto hizo zinakaribia kwisha kutokana na halamshauri yake kuweka nguvu katika kuzitatu.

‘ Tangu mwaka 2017 tumepokea zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni mia nane kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI katika mpango wa uboreshaji wa Miundo mbinu ya sekta ya Afya ambapo vituo vinne vya Afya vy... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More