Pancho Kuzikwa Gairo Mkoani Morogoro. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Pancho Kuzikwa Gairo Mkoani Morogoro.

Baba mzazi wa marehemu Pancho Latino amefunguka na kutangaza rasmi kuwa mtoto wake atazikwa katika kijiji chao kilichopo Gairo mkoani Morogoro .


Baba wa Pancho Latino anasema kuwa amesikitishwa sana na kifo cha mtoto wake ukizingatia kuwa aliweza kuongea nae hivi karibuni kbala ya kifo chake na hata alipoona katika mitandao kuhusu kifo chake alishangazwa sana na taarifa hizo.


Akielezea kwa undani kuhusu taarifa ya kifo hicho, baba wa marehemu anasema kuwa alianza kuona taarifa hizo katika mitandao na kisha kumpigia simu kaka yake aliyekuwa anakaa nae jijini Dar na ndipo alipothibitisha taarifa hizo.


Hata hivyo baba wa pancho ambae ni mchungaji wa kanisa moja mkoani hapo anasema kuwa mtoto wakeatazikwa siku ya jumamosi kama ratiba ilivyo na kama kuna mabadiliko yoyote pia watataoa taarifa zaidi.


The post Pancho Kuzikwa Gairo Mkoani Morogoro. appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More