Papa Francis 'ahofia' makasisi ambao ni wapenzi wa jinsia moja - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Papa Francis 'ahofia' makasisi ambao ni wapenzi wa jinsia moja


Pope Francis at the Vatican November 22, 2017.

Papa Francis ameonesha kusikitishwa na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kwa makasisiPapa Francis amesema mapenzi ya jinsia moja kwa makasisi ni "jambo kubwa" na ambalo linampa "hofu". Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani ametoa kauli hiyo katika mahojiano na Mmishenari kutoka Uhispania kuhusu wito wa kidini. Mahojiano hayo ni sehemu ya kitabu kinachoandikwa na mmishenari huyo. Papa amesema mahusiano ya jinsia moja ni jambo la "fasheni", na ametaka makasisi kutii viapo vyao vya utawa (kutojihusisha na mapenzi)
Gazeti la Corriere della Sera la nchini Italia limechapisha sehemu ya mahojiano hayo katika mtandao wake juzi Jumamosi. Papa Francis amesema kanisa katoliki linapaswa kuwa "imara" wakati wa kuchagua watu watakaokua makasisi. "Hili suala la mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja ni kubwa sana," amesema Papa na kusisitiza kuwa wale wote wanaohusika na mafunzo kwa makasisi wahakikishe kuwa wanafunzi wao "wamekomaa kibinaadamu na kihisia" kabla ya kuwapatia Sakramenti ya Upadre (upadrisho... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More