Pascal wa BSS afanyiwa upasuaji wa kibofu India, akutwa na tatizo lingine (Audio) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Pascal wa BSS afanyiwa upasuaji wa kibofu India, akutwa na tatizo lingine (Audio)

Mshindi wa BSS 2009, Pascal Kassian wiki hii amefanyiwa upasuaji wa kibofu cha mkojo nchini India baada ya kuugua kwa muda mrefu bila msaada mpaka pale Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda aliuvyojitokeza na kumsaidia.Muimbaji huyo ambaye alipata ajali mbaya ya gari na kusababisha kibofu chake cha mkojo kuaribika, aliondoka Dar es salaam Jumanne ya wiki hii na kufika India siku ya Jumatano.

Akiongea na mwandishi wetu, Pascal alisema baada ya kufanyiwa upasuaji wa kibofu, alikutwa na tatizo jingine na baada ya kupimwa alikutwa na mawe kwenye kibofu cha mkojo.

“Kwa sasa naendelea vizuri, baada ya kufanyiwa upasuaji wa kwanza bado nikawa na maumivu kwenye kibofu, lakini nawashukuru madaktari baada ya kunifanyiwa vipimo walikuta nina mame kwenye kibofu, nashukuru wameyaondoa,” alisema Pascal.


The post Pascal wa BSS afanyiwa upasuaji wa kibofu India, akutwa na tatizo lingine (Audio) appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More