PATAMU TAIFA LEO ‘TEAM SAMATTA V TEAM KIBA’ KATIKA MECHI YA HISANI KUCHANGIA VIFAA NA MIUNDOMBINU YA SHULE - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

PATAMU TAIFA LEO ‘TEAM SAMATTA V TEAM KIBA’ KATIKA MECHI YA HISANI KUCHANGIA VIFAA NA MIUNDOMBINU YA SHULE

Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
MCHEZO wa kirafiki wa Hisani utakaohusisha nyota mbalimbali wa soka wakiwemo wastaafu wakiongozwa na Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta na Mwanamuiki nyota nchini, Ali ‘King’ Kiba unafanyika leo jioni Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana mjini Dar es Salam, Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji, amesema kwamba mchezo huo uliopewa jina #Nifuate ni wa kuhamasisha uchangiaji wa vifaa na miundombinu mashuleni utakuwa ni baina yeye na rafiki zake dhidi ya mwanamuziki Ali Kiba na rafiki zake.  

“Ni mechi ya hisani ya Samatta 11 na Ali Kiba 11, nimechagua rafiki zangu na Ali amechagua rafiki zake. Ni mechi ya Hisani kama nyingine nyingi ambazo zimekuwa zikifanywa na wachezaji wakubwa,”alisema Samatta ambaye amewataka wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kwa sababu kutakuwa na burudani nyingine pia. 
Kwa upande Ali Kiba amesema kwamba amefurahi sana urafiki wake n... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More