Paul Pogba ajitoa kwenye mbio za kuwania Ballon d’Or ‘Hapana mimi sistahili tuzo hii’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Paul Pogba ajitoa kwenye mbio za kuwania Ballon d’Or ‘Hapana mimi sistahili tuzo hii’

Kiuongo wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba amesema kuwa hastahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or  na hivyo kuonekana kama anajitoa mwenyewe bila hata kuondolewa kutokana na idadi ya kura zitakazopatikana baada ya kupigwa.Pogba ni miongoni mwa majina 30 yaliyotajwa kwenye listi ya kuwania tuzo hiyo ya mchezaji bora wa dunia ambayo inatarajiwa kutolewa jijini Paris Desemba 3 mwaka huu.


Kiungo huyo amesema kuwa angependa kuona wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Ufaransa wakichukua tuzo hiyo ila yeye anaona hastahili.


Kuna jumla ya wachezaji saba wa timu hiyo ya Ufaransa waliyotajwa kwenye orodha ya watu 30 wanaowania Ballon d’Or akiwemo kiungo wa Chelsea, N’Golo Kante na mlinda lango wa Tottenham, Hugo Lloris wengine ni Kylian Mbappe wa Paris Saint-Germain, Antoine Griezmann anaekipiga Atletico Madrid, Raphael Varane wa Real Madrid na Karim Benzema.


“Pengine anaweza kuwa Grizou (Griezmann), Kylian (Mbappe) au Raph’... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More