PEPE REINA NDIYE KIPA BORA WA KIHISTORIA ENGLAND - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

PEPE REINA NDIYE KIPA BORA WA KIHISTORIA ENGLAND

KIPA wa zamani wa Liverpool, Pepe Reina ameibuka kinara wa kudaka mechi nyingi za Ligi Kuu ya England kihistoria.
Mspaniola huyo, ambaye kwa sasa anachezea AC Milan ya Italia, alicheza Anfield kati ya mwaka 2005 na 2013, akidaka jumla ya mechi 285 za Ligi Kuu wakati huo.
FourFourTwo imehesabu mechi ambazo makipa walidaka kufungwa katika Ligi Kuu ya England tangu mwaka 1992, ikiwahusisha makipa waliodkaa kuanzia mechi 50 tu.
Na ni Reina ambaye ameibuka kinara, akiwapiku walinda milango wengine hodari wakiwemo Edwin van der Sar na Petr Cech kwa asilimi yake 47.02 jumla ya kudaka bila kufungwa. 
Kipa wa zamani wa Chelsea anayedakia Arsenal kwa sasa, Cech amechukua Medali ya Fedha kwa asilimi zake 45.68, wakati Mholanzi Van der Sar amekamata nafasi ya tatu kwa asilimia zake 42.17.
Mwingine aliyeingia tano bora ni kipa gwiji wa Denmark, Peter Schmeichel (asilimia 41.29) na gwiji wa Arsenal, David Seaman (asilimia 40.70).
Kipa wa Tottenham na Chelsea, Mtaliano, Carlo Cudicini alidaka mechi 64 bil... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More