Pete ya dhahabu iliyopotea kwa miaka 12 yapatikana kwenye karoti - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Pete ya dhahabu iliyopotea kwa miaka 12 yapatikana kwenye karoti

Pete ya dhahabu ambayo ilipotea kwenye shamba la Dave na mkewe Lin Keitch miaka 12 iliyopita imepatikana kwenye karoti iliyokuwa imevunwa tayari kwa kupikwa.Lin Keitch mwenye umri wa miaka 69 ambaye ni mkazi wa Monkton Heathfield nchini Uingereza aliipata pete hiyo wakati alipokuwa akiosha mboga alizokuwa amevuna kutoka kwenye shamba hilo lililopo nyumbani kwake.Kwa mujibu wa tovuti ya The Sun, Lin Keitch amesema kuwa karoti hiyo ilizidi kukua huku ikiwa na pete hiyo.


Karoti ilikuwa inakuwa huku ikiwa na pete hiyo, ni nafasi pekee kwa zaidi ya milioni, na shindwa kuamini macho yangu. Tuliitafuta huku na kule hatukuipata.Lin alipewa pete hiyo na mumewe, Dave katika sherehe yake ya kutimiza miaka 40 na kupotezwa na binti yao, Sarah kwenye shamba hilo lililopo nyumbani kwao mwaka 2006.The post Pete ya dhahabu iliyopotea kwa miaka 12 yapatikana kwenye karoti appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More