PETER TINO AONGOZA MSAFARA WA TAIFA STARS KWENDA PRAIA KUIVAA CAPE VERDE IJUMAA KUFUZU AFCON 2019 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

PETER TINO AONGOZA MSAFARA WA TAIFA STARS KWENDA PRAIA KUIVAA CAPE VERDE IJUMAA KUFUZU AFCON 2019

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
GWIJI wa soka Tanzania, Augustino Peter Magali ‘Peter Tino’ amesafiri na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwenda mjini Praia nchini Cape Verde kwa ajili ya mchezo na weneyeji wao hao Ijumaa.
Taifa Stars imeondoka Alfajiri ya leo kwenda Praia ambako Ijumaa watakuwa wageni wa Cape Verde katika mchezo wa Kundi L kufuzu AFCON kabla ya kurejea Dar es Salaam kwa mchezo wa marudiano na wapinzani wao hao Oktoba 16.
Tino ni mfungaji wa bao lililoipa Tanzania tiketi ya Fainali pekee za AFCON mwaka 1980 zilizofanyika mjini Lagos nchini Nigeria.
Tino, mchezaji wa zamani wa African Sports ya Tanga, Pan African, Yanga za Dar es Salaam na Maji Maji ya Songea, alifunga bao la kusawazisha dakika ya 84 Uwanja wa Ndola katika sare ya 1-1 na Zambia kufuatia Alex Chola kuanza kuanza kuwafungia wenyeji dakika ya 43  Agosti 26 mwaka 1979.

Wachezaji wa Taifa Stars wakiondoka mjini Dar es Salaam Alfajiri ya leo kwenda Praia 

Na Taifa Stars ikafuzu kwa ushindi w... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More