Petit Man Afungukia Tetesi Za Kufulia Mpaka Kuweka Bondi Passport - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Petit Man Afungukia Tetesi Za Kufulia Mpaka Kuweka Bondi Passport

Mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva Petit Man Wakuache amefunguka na kukana tetesi zinaendelea kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefulia.


Petit Man ambaye ni mume wa Esma Platnumz dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amekana taarifa za yeye kufulia mpaka kuweka passport yake ya kusafiria rehani.


Kwenye mahojiano na Bongo 5, Petit amesema taarifa hizo ni za uongo na zinasambazwa na mtu ambaye ni mbaya wake ambaye anapenda tu kumchafua;Sijawahi kufanya kitu hicho ndio maana hata sikuwahi kukizungumzia kwa sababu hates wako wengi sana, kuna watu wengi wanachuki na maisha yangu lakini sio habari za kweli na sijawahi hata kuitwa na Migration kwaajili ya hiyo ishu”.Tetesi za Petit Man kufulia zilipamba moto hasa pale alipodaiwa kuweka ndani polisi baada ya kushindwa kulipa deni shilingi milioni 10.


The post Petit Man Afungukia Tetesi Za Kufulia Mpaka Kuweka Bondi Passport appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More