Picha: Wanne wafariki ajali ya gari Manyara, dereva wa basi akimbia - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Picha: Wanne wafariki ajali ya gari Manyara, dereva wa basi akimbia

Watu wanne akiwemo kondakta wamefariki na wengine 10 kujeruhiwa katika ajali ya basi la Arusha Express yenye namba za usajili T 750 BYQ iliyotokea katika eneo la Mlima Haraa, Kata ya Bonga wilayani Babati mkoani Manyara.Basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Arusha kwenda Mbeya ambapo kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Augustine Senga, dereva wa basi hilo amekimbia na jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo chake.Waliokufa na kutambulika ni pamoja na Nassib Ramadhani ambaye alikuwa ni kondakta, Salvatory Mwinsanzu, Laurence Mwajabala na Janefred Mushi.The post Picha: Wanne wafariki ajali ya gari Manyara, dereva wa basi akimbia appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More