Pique abwaga manyanga - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Pique abwaga manyanga

Gerard Pique ameamua kuachana na soka la kimataifa na kujikita zaidi na klabu yake. Amesema hana mpango wa kurudi tena Spain. Pique alifanya maamuzi mwaka 2016 kwamba mwaka 2018 lazima apumzike.


Amesema amechoka kupigania taifa lake huku baadhi ya mashabiki wakimzomea. Pique ni mmoja wa wachezani waliokuwa wakipigania uhuru wa jimbo la Catalan. Mapema hivi karibuni alikutana na kocha spain bwana Luis Enrique lakini akamweleza hana mpango wa kubadilisha maamuzi yake.


Baada ya mchezo wao kufuzu kombe la dunia dhdi ya Albania in Octoba 2016, amechoka kukejeliwa na kukosolewa kila mara.

Pique, 31, hakusema chochote mara baada ya kombe la dunia kutolewa mapema kabisa katika hatua ya 16 bora.


‘nimeongea na kocha Luis Enrique siku kadhaa zilizopita. Aliniambia atanijumuisha kikosini lakini nikamwambia msimamo wangu upo oale pale.


‘naomba niondoke kwa amani. Nimepigania taifa hili. Nakumbuka vyema mafanikio yetu ya kombe la dunia 2010. Kwa sasa imetosha” Alisema Pique
Timu ya taifa (Takwimu
2002–2003 Spain U16 7 (2)
2004 Spain U17 8 (3)
2006 Spain U19 8 (3)
2007 Spain U20 5 (1)
2006–2008 Spain U21 12 (1)
2009–2018 Spain 102 (5)
2004–2018 Catalonia 9 (0)


Mafanikio


 Spain
Kombe la dunia
Mshindi 2010
UEFA Kombe la Mataifa ya Ulaya
Mshindi 2012
FIFA Kombe la Mabara
Mshindi wa pili 2013
Pique amecheza micheo 102 kwa Spain , ameshinda mataji mawili, Europa mara 1 na kombe la dunia.


Source: Shaffih DaudaRead More