PLUIJM AIWEKEA MKAKATI MZITO LIPULI, AWAAMBIA MAPEMA WACHEZAJI WA AZAM WAJIPANGE - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

PLUIJM AIWEKEA MKAKATI MZITO LIPULI, AWAAMBIA MAPEMA WACHEZAJI WA AZAM WAJIPANGE

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Hans Van Der Pluijm, ametoa angalizo kwa wachezaji wake akisema kuwa inahitajika utayari kuelekea mchezo ujao dhidi Lipuli.
Mara baada ya Azam FC kumaliza mechi zake tatu za Kanda ya Ziwa, sasa itarejea nyumbani keshokutwa Alhamisi kuvaana na Lupuli katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi saa 1.00 usiku.
Azam FC ilihitimisha mechi za kanda hiyo, kwa kuichapa Alliance bao 1-0 lililofungwa na Tafadzwa Kutinyu, awali ilicheza michezo mingine miwili na kutoka sare dhidi ya Mwadui (1-1) na Biashara United (0-0).

Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, Pluijm amekiri ugumu wa wapinzani wao kuelekea mchezo huo huku akidai wanatakiwa kujiandaa vema ili kuweza kuvuna ushindi mwingine Alhamisi.
“Unajua kuwa kila timu dhidi ya Azam, wanacheza asilimia 50 zaidi ya mechi nyingine tunatakiwa kuwa tayari kwa ajili ya hilo na kujiandaa vema,” alisema.
Akitoa ... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More