PLUIJM ASIKITIKIA SARE YA JANA MWADUI, ASEMA; "TULISTAHILI KUIBUKA NA USHINDI" - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

PLUIJM ASIKITIKIA SARE YA JANA MWADUI, ASEMA; "TULISTAHILI KUIBUKA NA USHINDI"

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Hans van der Pluijm, ameweka wazi kuwa walistahili kushinda kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-0 jana dhidi ya Mwadui.
Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mwadui, ilishuhudiwa Azam FC ikijipatia bao lake kupitia kwa kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na kujipatia pointi moja ugenini iliyoifanya kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha pointi saba sawa na Mbao.
Pluijm amesema kwamba walistahili ushindi kutokana na timu yake kucheza vema huku akidai walijisahau dakika moja na wapinzani wao kutumia nafasi hiyo kusawazisha bao na kufanya mchezo kuisha kwa sare.

Hans van der Pluijm (kulia) akiwa na Msaidizi wake, Juma Mwambusi (kushoto) jana Mwadui

“Tulicheza vizuri sana, kwangu mimi kwa dakika 90 unatakiwa kucheza kwa umakini na nidhamu ya mbinu na tulijisahau dakika moja, nidhamu yetu na namna tulivyopaswa kucheza na wakapata bao ambapo kwa maoni yangu hatukurudi nyuma haraka na kip... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More