POGBA AWAAGA WACHEZAJI WENZAKE MAN UNITED ANAKWENDA BARCELONA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

POGBA AWAAGA WACHEZAJI WENZAKE MAN UNITED ANAKWENDA BARCELONA

KIUNGO Paul Pogba amewaambia wachezaji wenzake wa Manchester United kwamba anataka kuondoka Old Trafford kuhamia Barcelona.
Pogba amewafahamisha wachezaji wenzake hilo kiasi cha saa 48 zilizopita kwamba anataka kuuzwa, ikiwa ni miaka miwili tangu ajiunge tena United kutoka Juventus kwa dau la rekodi la Pauni Milioni 89.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 inafahamika amemtumia ujumbe wa maandishi wa simu ya mkononi Ed Woodward, akimfahamisha Makamu Mwenyekiti huyo wa United dhamira yake ya kuondoka, ingawa klabu imekana hilo.

Paul Pogba amewaambia wachezaji wenzake Manchester United anataka kuhamia Barcelona  

United imeendelea kusistiza kwamba Pogba hauzwi, kiasi cha siku mbili kabla kikosi cha Jose Mourinho hakijaanza msimu mpya wa Ligi Kuu ya England kwa kucheza na Leicester City. 
Watakuwa wana muda mfupi sana wa kusajili mbadala wake kabla ya dirisha la usajili kufungwa England Alhamisi Saa 11:00 jioni.
Sasa wanakabiliwa na changamo... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More