Polepole Awavaa Wapinzani..."Wameogopa Upepo wa Kisulisuli" - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Polepole Awavaa Wapinzani..."Wameogopa Upepo wa Kisulisuli"


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa watu wa vyama vya upinzani ni waungwana sana kwakuwa wameamua kujitoa wenyewe kwenye mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, baada ya kukiona chama hicho kilivyo imara na hawawezi kushindana nacho.

 Polepole amesema hayo leo Novemba 13, 2019, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

"Watu wa vyama vya upinzani ni waungwana, wametazama wakasema mambo yatakayotokea kwenye uchaguzi huu si ya mchezo, kwetu sisi ile 2014 inawezekana ulikuwa ushindi wa Tsunami ila wa mwaka huu utakuwa ni ushindi wa kisulisuli na ndiyo maana wakaamua kabla hatujafika pabaya wakaweka mpira kwapani. 


“Sisi ndiyo chama pekee wenye ilani ya chama inayotekelezwa, hata katika uchaguzi wa serikali za mitaa tumeandaa ilani ndogo ambayo itakuwa na mambo ambayo tutawaahidi Watanzania na tutayatekeleza,” alisema na kuongeza kwamba  CCM kimeweka  uzito mkubwa katika uchaguzi huu kwa sababu mambo ya maen... Continue reading ->Source: Mwanaharakati MzalendoRead More