POLISI DAR YAWAONYA WATAKAOFANYA VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI JIMBO LA UKONGA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

POLISI DAR YAWAONYA WATAKAOFANYA VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI JIMBO LA UKONGA


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetangaza kuimarisha ulinzi uchaguzi mdogo katika Jimbo la Ukonga na Kata ya Vingunguti unaotarajia kufanyika Septemba 16 mwaka huu.
Limesema halitamvumilia mtu yoyote  atakayebainika kufanya kuvuruga katika mchakato huo na kwamba atakeyakamatwa matokeo ya uchaguzi atayasikia akiwa mikononi mwa Polisi.
Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa wakati anazungumza namna walivyoimarisha ulinzi katika maeneo ambayo uchaguzi mdogo.
Amesisitiza jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa kutosha kabla, baada ya uchaguzi hadi matokeo yanapotangaza na mshindi kutangazwa.“Napenda kuwatoa hofu wananchi jeshi la Polisi limejiandaa kwa kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi huo.
“Tunawaonya waliopanga kufanya vurugu watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Rai ya jeshi la Polisi kwa wananchi ni kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa kufuata sheria na tarat... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More