POLISI INDONESIA WAOMBA MSAMAHA KWA KITENDO CHAKE CHA KUTUMIA NYOKA KUMBANA MTUHUMIWA WA WIZI YA SIMU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

POLISI INDONESIA WAOMBA MSAMAHA KWA KITENDO CHAKE CHA KUTUMIA NYOKA KUMBANA MTUHUMIWA WA WIZI YA SIMU

Na Ripota Wetu  JESHI la Polisi nchini Indonesia limeomba msamaha kwa kutumia nyoka kumtishia mtuhumiwa wa wizi baada ya video kusambazwa katika mitandao ya kijamii nchini humo. Baadhi ya maofisa wa jeshi hilo la polisi katika video hiyo wameonekana wakicheka na wengine waliokuwa wakimhoji mtuhumiwa huyo wakionekana kumuweka nyoka shingoni mwa mshukiwa huyo aliyekuwa amefungwa pingu huku akipiga kelele mashariki mwa eneo la Papua.
Habari iliyowekwa kwenye Mtandao wa Shirika la Habari la Uingereza(BBC) inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alifikishwa polisi kutokana na tuhuma za kuiba simu ya mkononi. Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo Tonny Ananda Swadaya amesema haikupaswa kufanyika hivyo lakini ametetea mbinu hiyo akieleza kwamba nyoka huyo hana sumu na kwamba wamechukua hatua kali dhidi ya maofisa waliohusika.
Swadaya amefafanua kuwa maofisa hao wa polisi hawakumpiga mshukiwa na kuongeza walichukua hatua kwa hiari yao kujaribu kumfany... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More