POLISI MOROGORO WATOA UFAFANUZI MWANAMKE ALIYEJIFUNGUA NJIANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

POLISI MOROGORO WATOA UFAFANUZI MWANAMKE ALIYEJIFUNGUA NJIANI

Na John Nditi, Morogoro
POLISI mkoani Morogoro inaendelea na uchunguzi zaidi kuhusu mwanamke aliyejifungua mtoto wakati akiwa njiani kupelekwa Kituo cha Afya Mang’ula, wilaya ya Kilombero mkoani humo mara baada ya kutolewa mahabusu ili kubaini kama kuna uzembe wowote umefanywa na watendaji ama askari na ikibainika hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Mugabo Wekwe alisema hayo katika taarifa yake kwa waandishi wa habari juu ya tukio la kujifungua mtoto njiani mwanamke Amina Rafael Mbunda (27) mkazi wa Kijiji cha Kiswanywa , Tarafa ya Mang’ula , wilayani Kilombero , mkoa wa Morogoro.Alisema , Polisi inaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio la mwanamke huyo aliyefikishwa katika kituo cha Polisi Mang’ula kwa kosa la kukutwa na mali ya wizi kisha kujifungua akiwa njiani kuelekea katika Kituo cha Afya Mang’ula.Alisema , Mei 31, mwaka huu ilifunguliwa kesi ya wizi wa samani mbalimbali z... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More