Polisi nchini Marekani wataka DNA ya Cristiano Ronaldo kuchunguzwa, kufuatia madai ya ubakaji - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Polisi nchini Marekani wataka DNA ya Cristiano Ronaldo kuchunguzwa, kufuatia madai ya ubakaji

Polisi mjini Las Vegas wametoa waranti ya kuchunguzwa kwa chembe chembe za vinasaba au DNA ya Cristiano Ronaldo kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya ubakaji dhidi ya nyota huyo wa kimataifa wa Ureno anayechezea klabu ya Juventus.

Kwa mujibu wa BBC, Wakili, Peter S. Christiansen, ameiambia BBC Michezo kuwa ombi hilo ”ni la kawaida”.

Jarida la Wall Street limeripoti kuwa waranti hiyo imewasilishwa hivi karibuni katika mfumo wa mahakama ya Italia.

Ronaldo amekanusha kwamba alimshambulia mwanadada Kathryn Mayorga katika mgahawa mmoja mjini Las Vegas hotel mwaka 2009.

”Bwana Ronaldo amekua akishikilia usemi kuwa yale yaliyotokea Las Vegas mwaka 2009 ni mambo ya watu wawili waliyokubaliana, kwa hiyo bila shaka chembe chembe za DNA zitapatikana, kwa hiyo sioni haja ya polisi kutoa ombi hilo kama sehemu ya uchunguzi wao,”ilisema taarifa ya Christiansen.

Gazeti la Der Spiegel la Ujerumani ambalo lilikuwa la kwanza kuangazia taarifa hiyo mwezi Oktoba, lilisema kuwa... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More