POLISI SABA WASIMAMISHWA KAZI, WAFIKISHWA MAHAKAMANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

POLISI SABA WASIMAMISHWA KAZI, WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Jeshi la Polisi Tanzania leo tarehe 11/01/2019, limewasimamisha kazi askari saba (7) wa vyeo mbalimbali kwa kutenda kosa kinyume na mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi na tayari wamefikishwa mahakamani kusomewa mashitaka yanayo wakabili. Hatua hii imechukuliwa, baada ya askari hao kuomba rushwa ya bilioni moja na baadae kupokea rushwa ya milioni mia saba toka kwa mfanyabiashara wa dhahabu aitwaye Sajid Abdalah Hassan ambaye walimkamata akiwa na dhahabu kiasi cha kilogramu 319.59, yenye thamani ya mabilioni ya shilingi za kitanzania.Askari hao waliosimamishwa kazi ni;E.4948 CPL Dani Isack KasalaF.1331 CPL Matete Maiga MisanaG.1876 PC Japhet Emmanuel LukikoG.5080 PC Maingu Baithaman SorrahG.6885 PC Alex Elias NkaliG.7244 PC Timoth Nzumbi PaulH.4060 PC David Kadama Ngelela.Aidha, kuhusu Afisa SSP: Moris Okinda ambaye alikuwa kiongozi wa askari hao walioomba na kupokea rushwa ya 
kiasi hicho cha fedha, mamlaka yake ya kinidhamu tayari imemsimamisha kazi na tayari amefikishwa mahakamani pamoja... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More